Mchezaji wa zamani wa Simba ajiunga na Mtibwa Sugar

89

Nahodha wa zamani wa klabu ya Simba aliyekuwa anakipiga kwa mkopo African Lyon, Hassan Isihaka amejiunga na klabu ya Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.

Hassan Isihaka alipelekwa kwa mkopo na Simba SC kunako klabu ya African Lyon baada ya kukosa namba ya kudumu klabuni hapo na anakuwa mchezaji wa tano kusainiwa na timu hiyo kwa msimu huu.

“Hassan Isihaka amejiunga na klabu ya Mtibwa Sugar akitokea Simba Sports, msimu 2016/2017 alikuwa African Lyon kwa mkopo na msimu huu amejiunga na wana tam tam baada ya kumsajili moja kwa moja akitokea Simba Sc”,Imeeleza taarifa kutoka kwenye mtandao wa klabu ya Mtibwa Sugar.

 

Weka maoni