Mgombea urais aahidi kutokomeza njaa Rwanda

168
Frank Habineza, mwasisi na mwenyekiti wa chama cha Democratic Green Party of Rwanda

Mgombea wa chama cha upinzani cha Green nchini Rwanda Dr. Frank Habineza amesema kama atashinda uchaguzi wa tarehe 3 na 4 mwezi Agosti ataondoa tatizo la njaa.

Leo (Alhamisi) Bw Habineza amezinadi sera zake wilayani Karongi Magharibi mwa Rwanda, na Huye Kusini mwa Rwanda.

Katika kampeni zake amesema atadhibiti hali ya usalama ili nchi iendelee kuwa na ulinzi wa kutosha.

Mbali na kudhibiti usalama, mgombea huyo amesema kitu cha kwanza atakachowafanyia wanyarwanda kama watamchagua, ni kuondoa tatizo la njaa.

Aidha Bw Frank Habineza amesema atawaongezea mishahara wafanyakazi wa serikali na kuboresha sekta ya kilimo.

Miongoni mwa watu waliofuatilia kampeni za mwanasiasa huyo, wamesema sera zake ni nzuri, na kama zitafanyiwa kazi zitawanufaisha wanyarwanda wengi.

Hii leo mgombea wa chama cha RPF-Inkotanyi Paul Kagame, amenadi sera zake wilayani Rulindo Kaskazini mwa Rwanda na Nyarugenge jijini Kigali.

Maelfu ya watu walifurika kwa wingi kwa ajili ya kampeni za rais Kagame wilayani Rulindo, ambapo mlima jirani ulikuwa umewekwa michoro ya jina la chama chke cha FPR (RPF) – Inkotanyi.

Mgombea huru Philippe Mpayimana ameshinda maeneo ya Rubavu Magharibi mwa nchi, akiwataka raia wampe kura zao.

Hali haikuwa nzuri kwa Mpayimana ambaye alipofika mjini Rubavu alikosa watu sehemu iliyokuwa imeandaliwa na uongozi wa wilaya, na hapo ndipo akaamua kwenda Mahoko akiwa anaulaumu uongozi wa wilaya kwa kumandalia sehemu ambayo hakuna watu wakati alitakiwa ajitafutie mwenyewe kunako makundi ya watu
Mpayimana alikosa mtu wa kumhutubia, kitu ambacho kilimkasirisha. Viti vya wageni wake vilibaki kama vilivyoletwa bila mtu wa kukaa

Weka maoni