Michezo ya VPL yabadilishwa kupisha mechi ya kirafiki ya Taifa Stars

367

Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko ya ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa baadhi ya mechi ili ziweze kupisha mchezo wa kirafiki baina ya Taifa Stars dhidi ya Botswana.

Mechi ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni kati ya  Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea; Azam FC na Simba, Njombe Mji na Young Africans; Mtibwa Sugar na Mwadui FC, Lipuli na Stand United; Singida United na Mbao; Kagera Sugar na Ruvu Shooting wakati Mbeya City na Ndanda FC ambazo sasa zitachezwa Septemba 6, 2017.

Michezo mingine ambayo imesogezwa hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na Kagera Sugar wakati Mbao na Tanzania Prisons utachezwa Septemba 21, mwaka huu.

Kadhalika mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United.

Tarehe hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.

Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba.

Kwa upande mwingine, Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani mwishoni  mwa juma hili kuvaana na timu ya Botswana katika mechi ya kirafiki itakayopigwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Weka maoni