Miss Mutesi Jolly ampa tano Kagame na chama tawala

179

Miss Rwanda 2016 Mutesi Jolly amewatolea mwito vijana kumchagua Paul Kagame ambaye anasaka mhula wa tatu kwa tiketi ya chama cha RPF-Inkotanyi.

Image result for miss rwanda mutesi jolly 2016

Mrembo huyo amesema Rais Kagame na chama chake cha RPF-Inkotanyi wamefanya kila kilichokuwa ndani ya uwezo wao kuhakikisha jamii inastawi.

Ametoa kauli hii wakati Wanyarwanda wakijiandaa kumchagua mtu wa kukikalia kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 3-4 mwezi ujao.

Katika mahojiano na RBA, msichana huyo amesema “vijana ndiyo nguzo za nchi. Kipi Rais Kagame hajatufanyia? Ni bahati gani alitunyima?”

Miss Jolly amewataka vijana wote wammiminie kura zao Paul Kagame ili aweze kuwasaidia kufanikisha mipango yao katika kipindi cha miaka saba ijayo.

Miss Jolly na Elsa Iradukunda ambaye ni Miss Rwanda 2017 wamekuwa wakionekana katika kampeni zinazoendelea za Kagame ambazo zilianza rasmi Julai 14.

Kagame ana washindani wawili: Frank Habineza wa chama cha Green Party na Philippe Mpayimana ambaye ni mgombea huria.

Weka maoni