Miss Queen Kalimpinya awakaba koo wavaa vimini

612

Aliyevishwa taji la mrembo namba tatu kwenye kinyang’anyiro cha Miss Rwanda 2017, Queen Kalimpinya, amewataka wasichana wenzie waache kuvaa nguo fupi.

Amesema anaamini hiyo itasaidia kupunguza mimba ambazo baadhi yao wanatungwa bila kutarajia, ambapo wengine hufariki wakati wa kujifungua.

Mrembo huyu ambaye ana umri wa miaka 18, amewanyooshea kidole wasichana ambao huvaa vimini kuwashawishi wanaume akisema mwisho wa siku uvaaji wao huwaponza.

“Kila siku hufanywa orodha za wasichana waliobebeshwa mimba zisizotarajiwa na wakiwa bado ni wadogo, wasichana wanatakiwa watunze heshima yao kwa kujisitiri kimavazi siyo kuvaa uchi wakidhani wamepiga umaridadi,” amesema Miss Kalimpinya.

Baadhi ya wanaume wanaofanyia shughuli zao mjini Kigali, wameusifia ushauri wa mrembo huyo, wakisema wasichana ndio wana ufumbuzi wa tatizo la mimba wanazobeba kwani hawabakwi.

Mmoja wao amesema msichana anapovaa mvao wa kuwatega wanaume anawapata, ila akishafanya hivyo mara nyingi hujisahau na kufanya ngono bila kutumia kinga.

“Msichana akivaa uchi unahamasika kama mwanaume, wapo ambao wanahimili hali hiyo ila wengine hushindwa kujimudu, utampa hela uburudike naye…,” amesema Hamimu.

Image result for miss kalimpinya queen

Wasichana 17500 wenye umri wa miaka 16-19 walitungwa mimba mwaka jana tu, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Usawa wa Jinsia na Ustawi wa Jamii (MIGEPROF).

Weka maoni