Mo Farah ayaaga mashindano ya Uwanjani kwa ushindi

103

Mwanariadha raia wa Uingereza, Mo Farah ameyaaga vyema mashindano ya kukimbiza upepo ndani ya uwanja baada ya kufanya vizuri Jijini Zurich katika mbio za mita 5,000 michuano ya Diamond League.

Farah alikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa bingwa wa dunia raia wa Ethiopia, Muktar Edris lakinia akafanikiwa kushinda kwa muda wa dakika 13 na sekunde 06.05.

Mo Farah mwenye umri wa miaka 34, ambaye ni mshindi wa wa mataji manne ya Olimpiki ameamia upande wapili wa mbio za  nje ya uwanja

“Nilihitaji kushinda, na hatimaye ninafuraha sasa ijapokuwa ilinibidi kupambana mpaka kupata ushindi huo, nitazimisi sana mbio hizi za uwanjani”, amesema Farah.

Kijana huyo  kutoka Uingereza ni mshindi wa Medali ya dhahabu katika mbio za ubingwa wa dunia wa mita 10,000  huku akipoteza taji la mbio za mita 5,000 alilokuwa akilishikilia.

Weka maoni