Mrembo Jokate Mwegelo alamba shavu CCM

177

Muigizaji na mjasiriamali kutoka Tanzania mrembo Jokate Mwegelo ameteuliwa na Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi, UVCCM, kuwa Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa jumuiya hiyo.

Kamati ya utekelezaji ya UVCCM iliyokutana jana imemteua Jokate Mwegelo na wenzake wanne kwenye kada tofauti tofauti huku Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamid Shaka akiwasisitizia waandishi wa habari kuwa ana imani nafasi hiyo inabaki kuwa deni na chachu ya kujitoa kwa nguvu zake zote, kwa akili zake zote kuitumikia vizuri nafasi hiyo.

Kamati ya utekelezaji ya UVCCM Taifa iliyokutana katika kikao chake cha tarehe 18/04/2017 Upanga jijini dar es Saalama pamoja na mambo mengine kwa mamlaka waliyonayo kikanuni  Ibara ya 88,Idara za Umoja wa Vijana wa CCM  na Ibara ya 89 Uteuzi wa Wakuu wa Idara za Makao Makuu Uk 116ilikaimisha nafasi zote za Idara ili kukamilisha Muundo wa Kamati Tendaji ya UVCCM (Sekretariet) kama ifuatavyo:

Ndg Dorice H. Obeid – Idara Uchumi, Uwezeshaji na Fedha.

Ndg Daniel M. Zenda – Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu

Ndg Jokate U. Mwegelo – Idara Uhamasishaji na Chipukizi

Ndg Mohamed A. Abdalla – Idara ya Organization, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Ndg Israel Sostenes – Idara ya Usalama na Maadili

Mbali na hilo Shaka Hamid amewataka vijana wa CCM kupuuzia uvumi kwamba uchaguzi huo ulikuwa na mizengwe badala yake kuamini kile kinacholezwa na viongozi wa jumuiya hiyo.

 

Weka maoni