Msanii Amani wa Kenya afunga ndoa kwa siri

377
Msanii Amani

Msanii kutoka nchini Kenya Cecialia Wairimu maarufu kama Amani ambaye pia aliwahi kuwa mpenzi wa msanii wa Bong Flava, AY ametaja sababu za ukimya wake wa muda mrefu katika muziki.

Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Post, umesema sababu ya ukimya huo wa Amani ni kutokana na kufunga ndoa ya siri na mumewe ambaye ni raia wa Nigeria anayefanya kazi nchini Kenya kama Mkurugenzi wa kikanda wa tawi la kampuni ya simu ya Tecno.

Amani na mumewe

“Nimesha olewa. Ni mke wa fulani sasa. Najua wengi wanasubiri harusi lakini napenda maisha ya faragha sana,” amesema Amani, kwa mujibu wa Bongo5.

“Ndio maana hamnioni nikifanya mahojiano nikiwa nyumbani kwangu sehemu zingine kama hizo,” ameongeza.

Amani ni msanii ambaye si mpya kwenye ulingo wa muziki nchini Kenya, hasa ikizingatiwa kuwa aliachia santuri yake mnamo mwaka 2006.

Alitwaa tuzo lukuki za muziki ikiwemo zile za MTV Africa Music Awards,  Pearl of Africa Music Awards, Kisima Awards and Chaguo La Teeniez Awards.

Weka maoni