Msanii Knowless na mtangazaji Klepy wavaana Instagram kisa wizi

733
Knowless (kushoto) na Klepy

Hapo jana Jumanne msanii wa kike nchini Rwanda Butera Knowless aliamua kum-block mtangazaji Klepy katika mtandao wa Instagram baada ya mtangazaji huyo kuikosoa cover ya wimbo wake wa Winning Team.

Wimbo ambao bado haujatoka, Knowless aliposti cover yake kwenye mtandao wa Instagram kuwafahamisha mashabiki anachowapikia, na hapo ndipo akakaribishwa na madai ya wizi wa cover ya nguli wa muziki wa Marekani.

Cover hiyo ilikuja kuzua utata baada ya mtangazaji Muneza Klepy Bertrand kuweka maoni yake akisema kuwa Knowless aliiga cover ya santuri ya ‘Major Key’ ya Dj Khaled.

Mtangazaji wa Contact FM Muneza Klepy.

 

Hayo ndiyo maoni ya Klepy akiibua mazito kuhusu cover ya wimbo wa Knowless

Knowless hakufurahishwa na kitendo cha Klepy kumuambia kuwa ameiga cover ya albamu ya Dj Khaled.

Baada ya muda usio mrefu Knowless alionekana kupuuzia kauli ya Klepy kwa kumuambia ‘so what?’, akitaka kumaanisha kuwa mtangazaji huyo ameongea upuuzi.

Malumbano yaliendelea kwani Klepy naye alirudi na kuandika “Create something new”, akimshauri msanii huyo ajiongeze, awe mbunifu na siyo kuiba covers za albamu za wasanii wenzake.

 

Knowless alikerwa na majibu ya Klepy na kuamua kufuta maoni yote ambayo mtangazaji huyo alikuwa ameweka, na kisha kumzawadia block ili asiendelee kumsumbua.

Baada ya mtangazaji huyo kublokiwa alihamishia silaha zake Facebook, ambapo aliwaeleza marafiki zake yaliyomsibu kutokana na ushauri wake juu ya cover ya wimbo wa Knowless.

Amesema Knowless hakutakiwa amblock kisa amemshauri kuwa mbunifu kwani msanii anahitaji kuwatega sikio wanaoongea kuhusu kazi zake ikiwemo watangazaji.

 

 

Mmoja kati ya marafiki wa Klepy alimuunga mkono na kusema wasanii wanapenda watangazaji wanaowasifia na siyo wale wanaowarekebisha.

Mtoa maoni alisema kuwa Knowless kuiga cover ya Dj Khaled wala si jambo la kushangaza kwani hata jina lake la Knowless alichukua kutoka kwa Beyonce Knowless.

Weka maoni