Msanii Mani Martin mapenzini, hivi ndivyo vigezo alivyokidhi mpenzi wake

243
Msanii Mani Martin

Kuolewa kwa Najim kuliwafanya waliomjua kama mpenzi wa msanii Mani Martin wabaki wameduwaa na kuendelea kujiuliza kilichomfanya amkimbie msanii huyo.

Akiongea kwenye kipindi cha Ten Tonight cha Radio 10, Msanii Mani Martin amefunguka na kusema kwa sasa ana mpenzi ambaye hakutaka kumtaja kwa jina.

 

mani martin

Mani Martin ni msanii ambaye ana mazoea ya kutunza hisia zake, si mara nyingi anaonekana hadharani akiponda raha na mpenzi wake kama mastaa wengine.

Akiongea kuhusu mpenzi wake huyo, amefunguka kuwa, “Mimi bado ni kapera ila sipo peke yangu, nipo mapenzini na mtu. Sina mpango wa kuoa hivi karibuni ila sitaendelea kuishi kibachela”

Baada ya kuongea hayo, Martin amevitaja vigezo anavyotakiwa akidhi mpenzi wake kuwa:

  • Anatakiwa awe ni mtu anayetambua majukumu yakena anapigania maendeleo yake
  • Msichana ambaye anakazana apate chake na si kusubiri kupewa kila kitu na mumewe
  • Msichana mrembo ambaye kimaumbile amekamilika kila idara

Najim ambaye alikuwa anadaiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na nguli huyu wa muziki wa miondoko ya Afrobeat nchini Rwanda, alikuja kuolewa baada ya kuonekana kwenye video ya wasanii wengi.

Si Najim tu ambaye alisemekana anapendana na Mani Martin kwani hata Princess Priscillah aliwahi kukabiliwa na madai kama hayo, Priscilla akiwa ni msanii wa Rwanda ambaye anakaa Marekani.

 

undefined

 

Weka maoni