Msanii Miss Jojo afanyiwa bridal shower na mashoga zake

513

Baada ya kufunga ndoa ya kiserikali na mumewe saleh mnamo Machi 2017, msanii Miss Jojo amefanyiwa bridal shower na marafiki zake wa kike wakati akisubiri ndoa ya kidini.

Bridal Shower ni tafrija inayolenga hasa kumuelimisha bi harusi mtarajiwa kuhusu maisha ya ndoa, lakini pia kumsaidia kiuchumu ili aweze kufanikisha harusi yake.

Uwineza Josiane ambaye alijizolea umaarufu kwenye muziki kwa jina la Miss Jojo kupitia nyimbo zake zilizopendwa kama Siwezi enda, Mbwira, Ubona ko ndinde, ataoana kidini na mumewe huyo tarehe 29 Julai, 2017.

Inatarajiwa kuwa harusi hiyo itafanyika maeneo ya Rugenge wilayani Gasabo jijini Kigali, nikufahamishe kuwa bridal shower yenyewe ilifanyika nyumbani kwake Gikondo.
Pamoja na kwamba alikuwa na nyimbo pendwa, Miss Jojo aliamua kuweka kando shughuli za muziki mwaka 2013 akisema anataka kwanza akamilishe mipango yake binafsi.

Kuanzia wakati huo mpaka leo hajatoa wimbo hata mmoja ila amewataka mashabiki wake wasifikirie kuwa ameamua kuachana na muziki milele.

Weka maoni