Mtangazaji Anita Pendo akanusha kumtelekeza mtoto wake Gahini

310
Mjamzito Anita Pendo akiwa na mpenzi wake Ndanda

Mshereheshaji na Mtangazaji wa Kituo cha Habari cha Rwanda (RBA), Anita Pendo ametoa ya moyoni kuhusu mtoto wake anayedaiwa kumtelekeza kwao Gahini huko Kayonza.

Mjamzito huyo amesema huwa inamkera kuona watu wanasema eti ana mtoto aliyemuacha kijijini wakati anajua hajawahi kujifungua, na kuwataka wachunguze vizuri wanayoyasema.

“Ngoja nieleze kitu komoja, nimeona watu wakiniandika eti kuna mtoto nilimtelekeza Gahini, sina mtoto Gahini! Ambao mnaandika mfikiri na mchunguze vizuri ukweli halisi wa mambo,” ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Napenda watoto siwezi nikamficha mtoto nikiwa naye kwani mtoto ndo fahari ya mzazi, kwa hiyo ngojeeni ambaye Mungu atatujalia vingine muache, mtoto yuko njiani anakuja,” ameongeza.

Anita Pendo amethibitisha tetesi ambazo zimekuwa zikizagaa mitandaoni kuhusu ujauzito wake ambapo amekiri kuwa na mimba ingawaje hakuelezea ukubwa wake.

Amekuwepo katika mahusiano ya kimapenzi na golikipa maarufu wa timu ya soka ya AS Kigali, Nizeyimana Alphonse almaarufu Ndanda, ikiwa ni baada ya kumwagana na produza David.

Hiki ndicho alichokiandika Anita kumtakia sikukuu njema ya kuzaliwa mpenzi wake Ndanda

Anita Pendo amejizoolea umaarufu katika kupitia matamasha mbalimbali ya muziki ambapo anahudumu kama mshereheshaji, huku akiwa mtangazaji wa TV ya taifa na Magic FM pia.

Anita Pendo na mshereheshaji mwenzake Tino wakiwachangamsha wapenzi wa muziki kwenye tamasha la PGGSS mnamo Mei 2015 wilayani Ruhango

Weka maoni