Mtangazaji Mama Eminente ahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 3 jela

740
Mama Eminente

Mugabushaka Jeanne de Chantal aliyejizolea umaarufu nchini Rwanda kwa jina la Mama Eminente, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu na miezi miwili kwa makosa ya utapeli.

Mbali na kifungo hicho, Mahakama ya Mwanzo ya Kacyiru imeamua alipe hata faini ya faranga miliyoni 3.

Bizimana Ibrahim ambaye walishtakiwa katika kesi moja, naye amepewa adhabu kama hiyo ya kutumikia kifungo cha miaka zaidi ya mitatu na kulipa faini ya faranga miliyoni 3.

Mama Eminente alitiwa nguvuni mnamo Novemba 27, 2016, akikabiliwa na tuhuma za kuwalaghai watu kwa ahadi za kufanikisha usajili na utambuzi wa makanisa yao serikalini.

Mama Eminente ametupwa jela kumalizia miaka mitatu na miezi miwili

Jina la Eminente ni kubwa kwenye fani ya utangazaji nchini Rwanda, ambapo alivitangazia vyombo mbalimbali vya habari kwa nyakati tofauti ikiwemo Radio 10 na TV10.

Alionekana pia akiwa kwenye jopo la majaji katika kinyang’anyiro cha kusaka mlimbwende wa kuvishwa taji la urembo ambacho hufanyika kila mwaka kijulikanacho kama Miss Rwanda.

Mama Eminente akimpa kura ya ‘ndiyo’ mgombea wa Miss Rwanda

Wazo moja

Weka maoni