MTN yagoma kusema lolote kuhusu faini iliyopigwa na RURA

319

Kampuni ya mawasiliano nchini Rwanda imegoma kusema lolote kuhusu faini ya faranga zaidi ya bilioni 7 iliyotozwa na Shirika la udhibiti wa vyombo vya mawasiliano nchini RURA kwa kosa la kukiuka masharti.

MTN  ililazimishwa kulipa faini hiyo kutokana na kile kinachodaiwa kwamba, baadhi ya huduma za mawasiliano ambazo zilitakiwa kuendeshwa nchini Rwanda, zilipelekwa nje ya nchi hali inayohisiwa kuwa inaweza kuwapa mwanya wadukuzi kuingilia mambo nyeti ya taifa.

Nimejaribu kuwasiliana na uongozi wa MTN kwa takribani wiki nzima bila mafanikio yoyote.

Weka maoni