Mukabunani afungukia mchango wa mwanachama, sakata la Rwigara

318
Mukabunani Christine, Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha PS-Imberakuri

Asilimia tano ya mshahara wa kila mwezi ndio mchango wa mwanachama wa chama cha PS-Imberakuri, kiongozi wa chama hicho Bi Christine Mukabunani amesema.

Mwanachama ambaye hana kazi hutoa mchango wa faranga mia moja kwa mwezi, kwa mujibu wa kiongozi wa chama hicho.

Bi Mukabunani amesema zinapohitajika pesa nyingi basi huwa na mchango wa pamoja maarufu kama harambee kwa kila mwana chama wa PS Imberakuri.

Amezungumzia pia sakata la Diane Rwigara anayekabiliwa na tuhuma za wizi wa sahihi za wanachama 34 wa chama cha PS-Imberakuri bila wanachama hao kujua.

Rwigara ambaye azma yake ya kugombea urais iligonga mwamba, anadaiwa kuiba hizo ili kujaza sahihi za watu mia sita zinazotakiwa kwa wagombea huria.

Mi Mukabunani amesema kuwa bado wanafanya uchunguzi thabiti ili kuweza kujua kwa kina ni nani aliyempa nyaraka hizo kutoka katika chama chao.

Pia Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema Diane Rwigara aliwasilisha kwa tume hiyo sahihi za watu ambao walifariki dunia.

Mmoja wa watu hao alikufa kwa ugonjwa katika Hospitali ya Kibagabaga na kuzikwa katika makaburi ya Busanza, kwa mujibu wa maelezo ya NEC.

Uchunguzi utakapokamilika na kubainika alipotoa nyaraka hizo, basi wanaweza wakamfikisha mbele ya mahakama na kujibu tuhuma zinazomkabili.

Chama cha PS Imberakuri kilisajiliwa rasmi nchini Rwanda mwaka 2009, lakini hakijatoa mgombea katika uchaguzi wowote ule.

Aidha Bi Mukabunani amesema hivi sasa chama chake kimepiga hatua kidemokrasia na wanachama wake hawafungwi ovyo kama ilivyokuwa hapo awali.

Barafinda na Mwenedata waridhia uamuzi wa NEC

Weka maoni