Mwanafunzi aliyefanya kampeni kwa baiskeli ashinda ubunge Kenya

149

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu, John Mwirigi(24) ashinda Ubunge Jimbo la Igembe Kusini. Hakuchapisha karatasi za kampeni kutokana na kukosa fedha.

Aligombea kama mgombea binafsi na kumshinda Joseph Miriti kwa kura 18,659(39.09%) dhidi ya Joseph Mwereria wa Chama tawala cha Jubilee aliyepata kura 15,635(32.76%).

Vyombo vya habari vya nchini humo vinadai kijana huyo amefanya kampeni kwa kutumia usafiri wa baiskeli.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2001 Wananchi wa Meru walimchagua bwana Boniface Kinoti Gatobu kuwa Mbunge wa Jimbo la Buuri akiwa na umri wa miaka 26.

Kijana huyo anasoma mwaka wa tatu katika chão cha Mount Kenya University.

Weka maoni