Mwanamke wa kwanza atangaza nia ya kugombea urais Rwanda

1313
Diane Rwigara (Picha/Umuseke)

Diane Shima Rwigara, mtoto wa tajiri Asinapol Rwigara aliyeuawa mnamo mwaka wa 2015, ametangaza kuwa na nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti, 2017.

Mwanamke huyu anatarajia kukutana na waandishi wa habari hapo kesho Jumatano saa nane za mchana Jijini Kigali, ambapo ndipo ataeleza kinaganaga kuhusu azma yake ya kugombea kiti cha urais.

Umma umemjua Diane Rwigara hasa kutokana na matamshi aliyoyatoa kwa nyakati tofauti kuhusu kifo cha baba yake.

Jina lake ni geni kwenye ulingo wa siasa nchini Rwanda.

Amekuwa mwanamke wa kuanza kutangaza rasmi dhamira ya kuiongoza Rwanda kupitia uchaguzi mkuu unaokaribia.

Tume Huru ya Uchaguzi (NEC) imesema itaanza kupokea maombi ya kugombea urais ifikapo Juni 12, ambapo zoezi hilo litaendelea hadi tarehe 23 za mwezi huo.

Wengine waliotangaza dhamira ya kugombea urais ni pamoja na Rais Paul Kagame wa chama cha RPF-Inkotanyi, Frank Habineza wa DGPR na Philippe Mpayimana atakayesimama kama mgombea huru.

Wazo moja

Weka maoni