Mwandishi wa habari Ntamuhanga adaiwa kutoroka gereza kwa kuruka ukuta

115
Bw Cassien Ntamuhanga alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2015

Miongoni mwa habari ambazo zimezua gumzo nchini Rwanda ni mwandishi wa habari Cassien Ntamuhanga kutoroka Gereza la Nyamagabe kwa kuruka ukuta.

Mamlaka ya Magereza (RCS) imesema Bw. Ntamuhanga na wafungwa wenzake wawili wametumia kamba kupanda uzio wa gereza.

Ntamuhanga alikuwa mkurugenzi wa redio Amazing Grace mpaka alipotiwa mbaroni kwa makosa ya uhaini mnamo Aprili.

Alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela Januari 2015.

Msemaji wa RCS, CIP Hillary Sengabo amewataka wafungwa wengine ambao ametoka nao kuwa ni Batambarije Theogene na Sibomana Kirenge ambao hawana umaarufu wowote.

RCS imewataka wananchi kutoa taarifa polisi wakiwaona watatu hao ili warudishwe jela wakaendelee kutumikia vifungo vyao.

Weka maoni