Ni Kagame, wimbo mpya wa Bishop Matare unaomsifia Rais Kagame

640
Bishop Matare

Bishop Matare ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Ongea na Redio Salus cha Redio Salus inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Rwanda ametoa wimbo wa ‘Ni Kagame.

Ni wimbo unaolenga kuhamasisha wanyarwanda kumpigia kura rais Kagame katika uchaguzi mkuu wa urais utakaofanyika Agosti 2017.

Katika wimbo huo anatoa mifano hai ya maendeleo ya Rwanda chini ya Rais Kagame ambaye yupo madarakani kuanzia mwaka 2000 na anatarajiwa kushinda uchaguzi kuanza mhula wa tatu mwaka huu.

Bishop Matare ana jumla ya nyimbo tano tangu aanze kufanya muziki wa rap mwaka 2005.

Anasomea uandishi na mawasiliano Chuo Kikuu cha Rwanda.

Weka maoni