Nina kipaji cha kukomolewa kwenye mapenzi – Wolper

196
Jacqueline Wolper

Malkia wa filamu nchini Tanzania, Jacqueline Wolper amefunguka kueleza moja na sababu ya mahusiano yake na wanaume wengi kushindwa kudumu kwa muda mrefu.

Muigizaji huyo ambaye ameachana na msanii Harmonize miezi kadhaa iliyopita, amedai kuna baadhi ya wasichana wanaingilia mapenzi yake ili kumkomoa, kwa mujibu wa Bongo5

“Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipendae” alisema Wolper.

Licha ya Wolper na Harmonize kutoweka wazi sababu ya kuachana, lakini stori ambazo ziko mtaani zinadai Harmonize amemuacha muigizaji huyo baada ya kupata mwanamke wakizungu.

Ukiacha Harmonize, wanaume wengine ambao Jacqueline Wolper aliwahi kutoka nao kimapenzi ni pamoja na Abdallah Mtoro ‘Dallas’ na G. Modo.

Weka maoni