Picha: Hawa ndio mastaa walioshuhudia harusi ya Professa Jay

227

Msanii wa Hip Hop nchini Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Professa Jay, wikiendi iliyopita alifunga ndoa na mpenzi wake wa miaka 13 Grace Mgonjo.

Wawili hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph mjini Dar es salaam wakiwepo wasanii wenzake na wanasiasa wenzake pia.

Diamond Platnumz, AY na Harmonize ni miongoni mwa wasanii waliokuwepo harusini.

Ingawaje alikuwa ndiye bwanaharusi, lakini AY alipoimba mzuka ulimpanda Professa Jay na kumfanya anyanyuke ili kumsaidia kudondosha mistari ya rap.

Uchumba wa Professa Jay na Grace ulidumu kwa muda wa miaka 13.

A.Y kwenye harusi ya Professor Jay

Professor Jay akimuimbia mpenzi wake

Ilikuwa ni shangwe na furaha kwa waliokuwepo harusini

Harmonize akiwaimbia wapenzi hao

Diamond akiimba wimbo wa mapenzi

 

Weka maoni