Picha: Warembo 20 waliopita mchujo #MissRwanda2018

244
Hawa ndio walimbwende ambao wamepita katika mchujo uliofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Expo Ground ulioko tafarani Gatenga, wilayani Kicukiro mjini Kigali

Usiku wa kuamkia Jumapili ya Februari 4, 2018, ulikuwa ni wa furaha tele kwa wasichana 20 ambao wamepita katika mchujo wa kuelekea fainali ya Miss Rwanda 2018.

Baada ya kuulizwa maswali na kuyajibu kadri ya uwezo wao, jopo la majaji lilikaa na kuamua nani kati ya wasichana 35 waliochaguliwa kuiwakilisha mikoa na mji wa Kigali wanafaa kuendelea na safari ya kusaka taji la urembo na nani watupwe nje.

Jopo hilo limeundwa na majaji watatu ambao ni pamoja na Miss Rwanda namba mbili mwaka 2009 Rusaro Carine, Mtangazaji wa Kiss FM Sandrine Isheja Butera na Francine Uwera Havugimana kutoka shirikisho la taasisi binafsi.

Ushindi wa warembo hao umepatikana kwa kuangalia urembo (maksi 30), majibu ya maswali waliyoulizwa (maksi 40) na ustadi wa kujibu maswali (maksi 30).

Waliopata bahati ya kuendelea kuwepo shindanoni watachuana katika shindano la kukunja jamvi litakalofanyika katika ukumbi wa Kigali Convention Centre mnamo Februari 24, 2018.

Washindi wa mchuano wa usiku uliopita ambao wametajwa kupelekwa kambi ya mazoezi huko Nyamata wilayani Bugesera mnamo Februari 9, ni hawa wafuatao:

• Liliane Uwase Ndahiro.

Mrembo huyu amechaguliwa kwa njia ya kura za raia kwa kupata kura elfu 56 500. Kigezo cha wingi wa kura zilizopigwa kwa jumbe fupi za maandishi (SMS) tu ndio kimemfanya apite.

Liliane Uwase Ndahiro

Warembo wengine waliopita kwa vigezo vya urembo na kujibu maswali ni,

• Shanitah Munyana

Huyu ndiye Umunyana Shanitah. Jaji alimuuliza je, mtoto mdogo akikuuliza utamaduni ni nini utamjibuje?, akajibu eti ‘nitamjibu ni kutunza heshima na nitamshauri afanye kama mababu, awe shujaa na ajiheshimu.

• Irene Natasha Ursule

Irene Natashe Ursule

• Shemsa Munyana

Shemsa Munyana

• Karen Umuhoza

Karen Umuhoza

• Noriella Ishimwe

Ishimwe Noriella

• Liliane Iradukunda

Liliane Iradukunda

• Rebecca Umuhire

Rebecca Umuhire

• Fiona Uwase

Fiona Uwase

• Vanessa Irakoze

Vanessa Irakoze

• Anastasia Umutoniwase

Anastasie Umutoniwase

• Lydia Dushimimana

Lydia Dushimiyimana

• Belinda Ingabire

Belinda Ingabire

• Divine Ingabire

Divine Ingabire

• Belinda Uwonkunda

Belinda Uwonkunda

• Paula Umutoniwase

Paula Umutoniwase

• Solange Uwineza

Solange Uwineza

Picha na Inyarwanda

Kampuni ya Rwanda Inspiration Backup ndio imekuwa ikiratibu na kuongoza kinyang’anyiro cha Miss Rwanda tangu mwaka 2014, kibarua ilichonasa serikalini baada ya waandaaji wengine kuonekana kutetereka.

Tofauti na miaka iliyotangulia ambapo Miss angeweza kuwa na taji kwa zaidi ya mwaka mmoja, Rwanda Inspiration Backup imehakikisha anapatikana Miss kila mwaka.

Miss Rwanda namba mosi alichaguliwa mnamo Disemba 17, 1993 na anaitwa wera Delila. Ukiacha taji alilovishwa, alitunukiwa hata faranga elfu 50.

Uwera Delira ana rekodi ya kuwa mlimbwende namba mosi na alivishwa taji la urembo mwaka 1993
Miss Uwera ameolewa na Mbeljiji Dirk mwaka 2013. Wanakaa Ubeljiji.

Kutokana na machafuko ya kikabila ambayo yalipelekea kufanyika kwa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994, nchi iliingia matope na hakuchaguliwa Miss mwingine.

Mashindano ya urembo yalilala usingizi fofofo hadi mwaka 2009 ambapo Bahati Grace alichaguliwa kuwa Miss Rwanda, taji aliloshikilia kwa muda wa miaka mitatu.

Bahati Grace aliibuka kidedea Miss Rwanda 2009. Kutokana na kutofanyika kwa mashindano mengine ya umiss alishikilia taji hilo hadi mwaka 2012.

Kufuatia kutunga mimba na kujifungua mtoto akiwa bado ana taji husika, Bahati hakuruhusiwa kulikabidhi  kwa Miss Rwanda 2012 Mutesi Kayibanda Aurore kwani kupata mtoto nje ya ndoa ni kwenda kinyume na maadili ya jamii ya Rwanda.

Mutesi Kayibanda Aurore alinyakua taji la Miss Rwanda 2012.

Miss Aurore Kayibanda Mutesi alishiriki mashindano ya Miss Supranational na MISS FESPAM ambapo alitwaa taji namba mosi katika shindano hilo la Miss FESPAM mwaka 2013.

Mutesi Kayibanda Aurore alishikilia taji la urembo kwa muda wa miaka miwili kwani mwaka 2013 hakupatikana Miss Rwanda mwingine.

Mwaka 2013 hakukuwa na shindano la Miss Rwanda. Ikiwa na maana kwamba Mutesi Aurore aliendelea kuwa na hadhi ya Miss Rwanda.

Hiyo ilikuwa mpaka 2014 ambapo Rwanda ilimpata Colombe Akiwacu na hapo ndipo yakafanyika makabidhiano ya taji la urembo.

Miss Rwanda 2014 Colombe Akiwacu
Miss Akiwacu Colombe
Mwaka 2015 ilikuwa ni zamu ya Kundwa Doriane.
Miss Rwanda 2015 Doriane Kundwa
Miss Rwanda 2016 Jolly Mutesi
Jolly Mutesi, Miss Rwanda 2016
Jolly akiwa anamshughulikia Elsa Iradukunda baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro cha Miss Rwanda 2017
Miss Rwanda 2017 Elsa Iradukunda

Mkurugenzi wa Rwanda Inspiration Back up, kampuni inayoandaa mashindani ya Miss Rwanda, Ishimwe Dieudoné almaarufu Prince Kid, amesema warembo wanaochaguliwa kupitia Miss Rwanda huitangaza Rwanda kimataifa.

Amesema kuna watu wameijua Rwanda hasa kutokana na mauaji ya kimbari yaliyoighubika mwaka 1994 na leo ukiitaja Rwanda ndicyo kitu kinachokuja vichwani mwao.

Prince Kid amesema Miss Rwanda wakienda nje ya Rwanda mashindanoni huufahamisha ulimwengu kuwa Rwanda ya leo ni nchi ambayo imetulia kiusalama na ambayo wananchi wake wameshikamana kuleta maendeleo, tofauti na Rwanda ya mwaka 1994 wanayoijua.

Endelea kumakinika na Habari Pevu kwa habari za kuaminika kutoka Rwanda na kwingineko duniani kwa lugha adhimu ya Kiswahili.

Weka maoni