Rais Magufuli ni kiongozi mzalendo – Dkt Mpango

325
Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Mhe. Dkt Philip Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Philip Mpango amesema kuwa Rais Magufuli ni kiongozi mzalendo na anayependa kujivunia nchi yake ya Tanzania.

Dkt Mpango ameyasema hayo, bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi ya mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018, kwa mujibu wa Bongo5.

“Mimi naamini, na Bunge lako Tukufu na Watanzania walio wengi watakubaliana nami kuwa, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anazo sifa zote hizi.Ni kiongozi mzalendo , anayependa na kujivunia nchi yake ya Tanzania, ni kiongozi ambaye amejielekeza kuijenga Tanzania mpya; ana moyo thabiti,” alisema Dkt Mpango.

“Nia njema na kujifunga kuwatumikia Watanzania wote na hasa wanyonge, ana msimamo thabiti usioyumba, anayo dhamira ya dhati ya kusimamia utendaji uliotukuka, anachukia rushwa, ubadhirifu, ufisadi na wizi wa rasilimali za umma, ana uthubutu wa kufanya mambo mapya tofauti, yenye maslahi kwa Taifa kinyume na mazoea, hata kama hayawapendezi baadhi ya watu.”

Weka maoni