Rais Nkurunziza aondoka Burundi kwa mara ya kwanza tangu 2015

498
Rais wa Burundi Piere Nkurunziza alivyokaribishwa na rais wa Tanzania John Magufuli Julai 20 2017 wilayani Ngara

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameondoka nchini mwaka kwa mara ya kwanza tangu jaribio la kuipindua serikali yake kukwamishwa mnamo Mei 13, 2015.

Nkurunziza ameitembelea Tanzania ambapo amekaribishwa na mwenyeji wake wilayani Ngara, akiwa amesindikizwa na mawziri wengi, kwa mujibu wa Xinua News Agency.

Taarifa kutoka ikulu ya Burundi inaeleza kuwa ziara ya rais Nkurunziza imelenga kuimarisha mauhusiano baina ya nchi hiyo na Tanzania.

Jeneral Godefroi Niyombare alitangaza kumuondoa mamlakani rais Nkurunziza, wakati rais huyo akiwa mkutanono Dar es Salaam, Tanzania.

Hali hiyo iliingiza Burundi katika hali ya misukosuko ambapo malaki ya watu waliikimbia nchi hiyo kwa sababu za kiusalama.

Tanzania inahifadhi wakimbizi wa kirundi wapatao laki mbili, huku wengine wakiwa wapo Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Uganda.

Akiwahotubia wananchi, rais Nkurunziza amewaambia wakimbizi wanaoishi nchini Tanzania kurejea nyumbani ili kuijenga nchi yao, kulingana na RFI.

“Tunawaomba raia wa Burundi wanaoishi hapa nchini Tanzania, kurudi nyumbani ili tuijenge nchi yetu,” alisema.

Aidha, ameishukuru Tanzania kwa kuwa jirani mwema na kuwapa hifadhi raia wa Burundi waliokimbia nchi yao.

Rais Magufuli amesisitiza ujumbe wa rais Nkurunziza na kuwataka wakimbizi hao kuchukua hatua za kurudi nyumbani kwa hiari.

Weka maoni