Rais wa Algeria amfukuza kazi Waziri Mkuu wake Abdelmadjid Tebboune

99

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amemtimua kazi Waziri Mkuu wake Abdelmadjid Tebboune(71), ambaye aliteuliwa katika nafasi hiyo miezi mitatu iliyopita.

Baada ya kutimuliwa kazi Waziri huyo tayari jina la Waziri mpya limetajwa la Ahmed Ouyahia kumrithi ambaye alikuwa mnadhimu mkuu wa Rais. Hakuna sababu zilizotajwa za kufukuzwa kazi Tebboune.

Siku kadhaa Rais Bouteflika alimtumia barua kali Tebboune kutaka kufanyika mabadiliko ya sera.

 

 

Weka maoni