Rais wa FIFA Gianni Infantino aisifu Rayon Sports ya Rwanda

255
Infatino akiwa kwenye dimba la Amahoro nchini Rwanda wakati wa mashindano ya CHAN (Picha?Igihe)

Rais wa Shirikisho la kimataifa la soka (FIFA), Gianni Infatino, ameisifu timu ya Rayon Sports kwa kujinyakulia kombe la ligi kuu nchini Rwanda katika awamu ya nane.

Akiwa ziarani nchini Rwanda mnamo Februari 2017,  Infatino alishuhudia mechi dhidi ya timu ya Rayon Sports na Police Fc katika uwanja wa taifa wa Amahoro Stadium.

Baada ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda kujihakikishia kombe la ligi kuu, Infatino ameitumia barua ya kuipongeza.

Gianni Infantino amewasifu viongozi wa timu hiyo na wakufunzi na mashabiki wote wa timu ya Rayon Sports, kwa kazi ngumu waliyoifanya hadi kujinyakulia kombe la ligi kuu.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa “ninayo furaha isiyokuwa na kifani rohoni mwangu kuwatumia ujumbe huu, kwani kutwaa kombe ni matunda ya kujitoa kwa hali na mali.”

Infatino alifanya ziara ya kikazi nchini Rwanda Februari 25, 2017, ambapo aliweka jiwe la msingi patakapojengwa hoteli ya shirikisho la mpira wa miguu nchini Rwanda, FERWAFA.

Weka maoni