Rapa Da Queen arudi na wimbo mpya baada ya kimya cha miaka 3

237

Baada ya miaka mitatu ya ukimya, msanii Da Queen amerudi rasmi kwenye muziki na wimbo wake mpya wa Carlo ambalo ni jina la mtoto wake mdogo.

Da Queen ni msanii wa kike kutoka nchini Rwanda ambaye jina lake liliongezeja kwenye orodha ya marapa wa Rwanda mwaka 2010.

Alifanya vizuri miaka hilo kwenye fani ya muziki hasa baada ya kutoa wimbo wa Akandiko alioshirikiana na rapa wa kiume Rideman.

Baada ya wimbo huo kumsaidia kupata mashabiki kibao alitoweka kwenye sanaa za muziki mpaka juzijuzi aliporudi na wimbo wa Carlo ambalo ni jina la mtoto wake wa kiume.

Katika mahojiano na Habari Pevu, Da Queen amefunguka kuhusu sababu zilizomfanya aache muziki kwa muda wa miaka mitatu na ambacho kimefanya arudi kwenye gemu.

“Mwaka 2014 baada ya kuolewa nilikuwa na mipango mingi ya ikiwemo ile ya kuijali familia yangu, mume wangu na mtoto wangu na miaka hiyo sikuwa Rwanda kwani familia yangu inakaa Zambia, ilibidi niache muziki kidogo.”

“Kwa hiyo nawaomba mashabiki wasichukulie kama nimeamua kuacha muziki kabisa, ndio maana wameona nimeachia wimbo mpya wa Carlo ambalo ni jina la mwanangu.”

Wimbo wa Carlo umetengenezwa na produza Trackslayer.

Da Queen amesema ukiacha wimbo huo amejiandaa vizuri kutoa nyimbo nyingine katika siku za usoni kwa hiyo mashabiki wake wakae mkao wa kula.

Weka maoni