Rapa Riderman adatishwa na mapokezi ya mashabiki wake Uchina

293
Riderman

Wiki iliyopita rapa mahiri kutoka nchini Rwanda Riderman alipaa kwenda Uchina kuwaimbia mashabiki wake wanaoishi nchini humo.

Amesema alishangazwa sana na jinsi Wachina walivyostaajabishwa na jinsi anavyofuga nywele zake kama marasta.

Amesema Wachina walipagawishwa na staili yake ya nywele ambapo wengine walimsogelea na kuanza kugusa nywele zake kana kwamba ni kitu ambacho hawajazoea kukiona.

Kuhusu tamasha alilofanya nchini humo siku ya Jumamosi wikiendi iliyopita, Riderman amesema tamasha hilo lilikuwa na msisimko sana na lilihudhuriwa na watu wengi.

Gatsinzi Emery ‘Riderman’ anatarajiwa kurudi nchini Rwanda wiki hii ila bado hajatangaza siku.

Weka maoni