Rayon Sports yamsimamisha mechi mbili kocha wake kwa matokeo mabaya

263
Masoudi Juma amesimamishwa mechi

Kocha wa klabu ya soka ya Rayon Sports kutoka nchini Rwanda, Masudi Djuma, amesimamishwa mechi mbili kufuatia timu hiyo kuchabangwa mabao mawili kwa nunge na Rivers United ya Nigeria kwenye michuano ya CAF Confederation Cup.

“Tumemsimamisha mechi mbili kumkumbusha kuwa alifanya vibaya, baadaye ndipo tutachukua hatua nyingine,” kiongozi mmoja wa Rayon Sports amenukuliwa na Ruhago Yacu.

Katika michuano hiyo ya klabu bingwa barani Afrika, Rayon Sports haikufua dafu kusawazisha magoli mawili ya Rivers United, hivyo kushindwa kuingia kwenye hatua ya makundi.

Wachezaji wa timu ya Rivers Club kutoka Nigeria walioipa kichapo Rayon Sports ya Rwanda

Jioni ya leo (Jumatatu), Masudi amesema hata yeye amezisikia taarifa za yeye kumwaga unga lakini hajapewa barua rasmi kuthibitisha uamuzi uliochukuliwa dhidi yake.

Masoudi aliingia mkataba wa miaka mitatu na Rayon Sports mwaka jana baada ya yeye kujihakikishia Kombe la Amani (Igikombe cy’Amahoro, kwa Kinyarwanda).

Weka maoni