Rick Ross na Briana Camille wapata mtoto wa kike

204

Rapper kutoka Maybach Music Group(MMG), Rick Ross amebahatika kupata mtoto wake wa kwanza na mwanamitindo Briana Camille.

Licha ya kuwa wawili hao hawakuwahi kutangaza kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na wala hawakuwahi kuonekana pamoja ila wamebahatika kupata mtoto wa kike. Inaelezwa kuwa Camille alikuwa akimsapoti rapper huyo mara kwa mara na kupelekea watu kuhisi wapo katika mahusiano hayo.

 

Kwa sasa familia ya Boss wa MMG imekuwa na watoto watatu ambapo wawili ni wakeki na mmoja ni wa kiume, ambao ni Toie Roberts na William Roberts III.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu vimeeleza kuwa mtoto huyo amezaliwa siku ya Labor Day wikiendi iliyopita na tayari ameshaanza kupokea zawadi kutoka kwa baba yake.

Weka maoni