Runtown na Sheebah kufanya tamasha Kigali Septemba

321
Runtown

Wasanii wakali kutoka Nigeria na Uganda, Runtown na Sheebah Karungi, wanatarajiwa kuja nchini Rwanda kwa ajili ya tamasha ambalo linaandaliwa na ‘I Factory Africa’ litakalofanyika Septemba 23, 2017.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Runtown ambaye ni msanii mkubwa nchini Nigeria na hata Afrika nzima, amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula.

Katika uimbaji wake, Runtown anachanganya Hip Hop, RnB na Reggae.

Wimbo wake wa Gallardo aliomshirikisha Davido ndio ulichaguliwa kuwa wimbo bora wa mwaka 2014 kwenye kinyang’anyiro cha Nigeria Entertainment Awards.

Sheeban Karungi, msanii wa kike kutoka nchini Uganda naye atakuja rwanda kwa ajili ya shoo

Sheebah karungi alijizolea ustaa nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla kupitia kundi la densi la Obsessions alilojiunga nalo mwaka 2006, ambalo baadaye alilipa kisogo.

Weka maoni