Ruvu Shooting yaibipu Simba kuelekea ligi kuu Bara

130

Ruvu Shooting imesema kikosi cha Simba kilichocheza na Rayon Sports ya Rwanda, Jumanne wiki hii, hakina uwezo wa kuwafunga katika mechi yao ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara Agosti 26, mwaka huu.

Katika Tamasha la Simba Day, Simba iliifunga Rayon bao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku Simba ikiwatumia karibu asilimia 97 ya nyota wake wote watakaotumika msimu ujao wakiwemo kina Okwi na Niyonzima na Mghana Gyan ambao walikonga nyoyo za mashabiki wa timu hiyo.

Akizungumza na 5sports, Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kama kuna mashabiki wanakiona kikosi cha Simba ni kizuri, basi wamepotea kwani wao wanakiona cha kawaida kisichoweza kuwasumbua pamoja na mbwembwe nyingi katika vyombo vya habari hasa magazeti juu ya uwezo wa kikosi cha timu hiyo kwa sasa.

Bwire ametamba kuwa wataishushia kipigo kikali Simba watakapokutana kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu itakayoanza Agosti 26, mwaka huu kwakuwa wao wanakikosi kipana chenye damu changa tofauti na Simba ‘akibeza’ kuwasajili maveterani kama kina Bocco na Nyoni na wengine wengi.

Weka maoni