Rwanda: Sasa unaweza kufungua mashtaka kwa njia ya kielektroniki

162
Sam Rugege, Rais wa Mahakama ya Rufaa nchini Rwanda

Mahakama ya Rufaa nchini Rwanda imetoa taarifa kwa umma kuhusu mfumo wa kielektroniki wa kufungua mashtaka katika mahakama zote nchini.

Jaji wa mahakama hiyo ametaarifu  kuwa, mbali na kufungua mashtaka, njia hiyo inamwezesha raia kufuatilia mwendelezo wa kesi pia.

Mfumo huo wa IECM (Integrated Electronic Case Management) ambao ulikuwa unatumiwa na baadhi ya mahakama, umeanza kutumiwa na mahakama zote kuanzia leo Juni Mosi.

Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Sam Rugege, ametaarifu kuwa maelezo ya matumizi  kuhusu mfumo huo yanapatikana pia kwenye mtandao wa kijamii wa  Youtube.

 

Kwa maelekezo zaidi, bofya hapa uisome taarifa hiyo ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kinyarwanda.

Weka maoni