Rwanda yatuma rambirambi shambulio la kigaidi London

289
Waziri wa nchi za nje wa Rwanda, Bi Luoise Mushikiwabo.

Waziri wa nchi za nje wa Rwanda Bi Louise Mushikiwabo, amedai kusikitishwa na shambulizi lililogharimu maisha ya watu saba nchini Uingereza hapo juzi Jumamosi.

“Tumevunjwa moyo na kusikitishwa na mashambulizi ya London na mlipuko wa Kabul, na mashambulizi mengine, mioyo yetu iko pamoja nanyi,” amesema Mushikiwabo ambaye pia ni msemaji wa serikali ya Rwanda.

Kundi la kigaidi la Islamic State limekiri kuhusika na shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu 7 na kuwajeruhi wengine 48.

Watu walielekezwa kwenda katika eneo salama baada ya tukio la kigaidi mjini London

Polisi nchini Uingereza wanasema wanawafahamu magaidi watatu waliotekeleza shambulizi hilo na watatoa majina yao hivi karibuni, kwa mujibu wa RFI.

Wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa wanaume watatu walioendesha basi lao dogo na kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada wowote.

Watu kumi na mmoja wanashikiliwa kufuatia uvamizi wa polisi mashariki mwa London, kulingana na BBC.

“Katika  wakati  huu, tunaamini  kwamba  watu  sita  wameuwawa  pamoja  na  washambuliaji watatu waliopigwa  risasi  na  polisi,” amesema  kamishna  msaidizi  Mark Rowley, ambae pia  ni  mkuu  wa  kitengo  cha  kupambana  na  ugaidi nchini Uingereza.

Waziri  mkuu  Theresa  May  aliliita  shambulio  hilo  kuwa “tukio la kigaidi” na  alieleza “shukrani  zake nyingi” kwa  polisi  na  huduma  za  dharura, Deutch Welle imeripoti.

Waziri Mkuu Bi.Theresa May amesema nchi hiyo bado inakabiliwa na tishio la ugaidi, na hivyo maafisa wa usalama wanafanya kila kilicho ndani ya uwezo wao kuhakikisha kuwa shambulizi lingine halitokei tena nchini humo.

Weka maoni