RwandAir yatua Uingereza kwa mara ya kwanza (Picha na video)

368
Ndege ya RwandAir baada ya kufika uwanja wa ndege wa Gatwick nchini Uingereza

Saa


Jana saa 18:00 GMT ndege namba A330-300 ya Shirika la ndege la Rwanda la RwandAir imetua uwanja wa Gatwick International Airport, London.

Ubalozi wa Rwanda nchini Uingereza umesema ndege hiyo imewasili London salama salimini. Ilikuwa imebeba abiria zaidi ya sitini.

Ndege hiyo iliondoka Kigali saa tano kasorobo GMT.

Itakuwa inakwenda London mara tatu kwa wiki, uongozi wa kampuni ya RwandAir umesema.

Gatwick International Airport ndio wa pili kwa kutumiwa na abiria wengi nchini Uingereza.

Ndege hiyo ilikuwa inaendeshwa na rubani wa kike, Esther Mbabazi.

Safari za Kigali-London zinatarajiwa kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini Rwanda na hata kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na hivyo kuchangia maendeleo ya kiuchumi.

Wanyarwanda katika mitandao ya kijamii wanazungumzia kitendo hicho cha ndege ya Rwanda kuingia soko la Uingereza.

 

Weka maoni