RwandAir yazidi kupasua anga, kesho itaanza safari za London

530

Huduma za shirika la ndege la Rwanda la RwandAir zinazidi kushika kasi ambapo safari ya kwanza ya kuenda London inatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa.

Ndege ya RwanAir itatua uwanja wa Gatwick International Airport ambao ni wa pili kwa kutumiwa na watu wengi jijini London.

Ndege hiyo imepangwa kuondoka Kigali saa saba kasorobo za mchana saa za Rwanda, sawa na saa tano kasorobo GMT.

Ni ndege aina ya Airbus A330 ambayo imewekwa vifaa vya kuwezesha abiria kutumia huduma za intaneti.

Safari za Kigali-London zitakuwa zinafanyika mara tatu kwa wiki.

Hatua hiyo inatarajiwa kusaidia kuongeza wingi wa bidhaa ambazo hupelekwa nje au kuletwa kutoka mataifa ya nje sanjari na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini Rwanda.

Gharama ya usafiri ni kuanzia Dola 400 kwa kichwa.

Mwezi uliopita RwandAir ilianzisha safari za kwenda Mumbai.

Weka maoni