Senderi amkaribisha Kitoko kwa mbwembwe

218

‘Mzee wa vituko’ Senderi International Hit amemkaribisha msanii mwenzake Kitoko Bibarwa akimkumkubusha pia kuwa ndiye anaongoza muziki wa Afrobeat nchini Rwanda.

Kitoko ambaye anarudi nchini Rwanda kutoka huko Uingereza ambako amekuwa akiishi kwa miaka kadhaa, alipokuwa bado nchini humu alikuwa hasimu wa Senderi kwenye gemu la miondoko ya Afrobeat.

Akimkaribisha katika mtandao wa Instagram, Senderi amesema, “Hujambo msanii mwenzangu, karibu(ni) kabisa Kigali-Rwanda, bado nahifadhi lile kombe la Afrobeat ambalo uliwahi kutwaa, nimelishikilia kwa miaka mitatu na bado nakomaa na muziki, karibu sana tunakukumbuka sana.”

Kitoko Bibarwa amekuja kwa ajili ya dili la kuimba kwenye kampeni za urais za mgombea wa chama tawala cha RPF-Inkotanyi, Paul Kagame.

 

Matamshi hayo ya Senderi yametafsiriwa na wadau wa muziki kuwa alitaka kumfahamisha Kitoko kuwa tangu aende Uingereza Senderi amebaki ndiye mfalme wa muziki wa Afrobeat.

Senderi na Kitoko ni miongoni mwa wasanii ambao wanafanya vizuri kwenye ulingo wa muziki wa Afrobeat nchini Rwanda, ambapo wote wanakisaidia chama tawala kuzipigia upatu sera za mgombea wake Paul Kagame ambaye anasaka awamu ya tatu ya urais tangu aingie mamlakani mwaka 2000.

Kitoko Bibarwa alikwenda Uingereza mnamo Machi 2013 akisema anakwenda kwa sababu za kimasomo, ambapo alisomea siasa chuo kikuu nchini humo.

Bado tunamtafuta Kitoko tusikie ana lipi la kuongea kuhusu matamshi hayo ya Senderi

Weka maoni