Serikali ya Nigeria kusitisha utoaji wa Passport kwa wasio na vitambulisho vya uraia

113

Serikali ya  nchni Nigeria kupitia Wizara ya Uhamiaji Nigeria Immigration Service (NIS), imetoa taarifa kwa raia wake kuwa ifikapo mwaka 2018 haitampatia mtu yoyote Passport ya kusafiria endapo hatakuwa na kitambulisho cha uraia.

Kwa mujibu wa mtando wa Thisday umeeleza kuwa Mdhibiti Mkuu wa Shirika hilo Mohammed Babandede,  na Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasilano kwa  Tehama, nchini humo wamefikia hatua hiyo ambayo ilijadiliwa katika kikao kilichofanyika pamoja na National Identity Management Commission (NIMC),  na kufikia uwamuzi wa kufanya hivyo.

Weka maoni