Sheebah & The Ben – Binkolera (Video)

502
The Ben (kushoto) na Sheebah

Hiyo ndiyo video ambayo imedondoshwa na Sheebah Karungi msanii mkali wa kike kutoka nchini Uganda akishirikiana na nguli wa muziki wa RnB na Pop nchini Rwanda, The Ben.

Video ya wimbo huu ilitoka miezi mitatu iliyopita ikiwa imetengenezwa na produza kutoka Uganda aitwaye Nessim.

Audio ya Binkolera ilifanya vizuri na bado inaendelea kufanya vizuri maredioni na katika vilavu vya starehe mjini Kigali.

Wawili hao waliahidi kutengeneza video yake Afrika Kusini na ahadi imetimia.

Video hii imekupa na mapokezi mazuri katika vituo vya televisheni nchini Rwanda.

Ungana nasi katika mitandao ya kijamii usipitwe na habari ambazo zimekwenda shule kwa Kiswahili: Facebook, Twitter na Instagram

Weka maoni