Simba sasa kukabidhiwa Ngao ya Jamii mbele ya Azam

145

Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limerekebisha Ngao ya Jamii upya kwa ajili ya klabu ya Simba baada ya ile ya awali kukosewa kuandikwa baadhi ya maneno.

Mabadiliko hayo yamefanyika baada ya makosa yaliyofanyika Agosti 23 mwaka huu ya kimaandishi kwenye Ngao ya Jamii ambapo Simba waliibuka washindi na kukabidhiwa Ngao hiyo.

Ngao ya Jamii iliyotolewa kwa Simba iliandikwa ‘Community Sheild’ badala ya ‘Community Shield’ kitu ambacho kilizua mijadala kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea (TFF) kuomba radhi kwa wanafamilia wa mpira wa miguu nchini na kuahidi tukio kama hilo halitojirudia tena.

TFF kupitia afisa habari wake, Alfred Lucas ameionesha Ngao ya Jamii iliyofanyiwa marekebisho na kusema kuwa Ngao hiyo itakabidhiwa kwa Simba siku ya jumatano ya tarehe 6 Septemba kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC.

Weka maoni