Simba yawafunga timu ya Rayon Sports FC ya Rwanda

129

Timu ya Simba imefanikiwa kuichakaza timu ya Rayon Sports FC ya Rwanda bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyofanyikia kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam jana jioni.

Bao hilo la ushindi limefungwa na mchezaji Mohamed Ibrahimu kwenye dakika 15 za kipindi cha kwanza cha mtifuano huo na kupelekea Simba kuwa mbele kwa goli moja dhidi ya Rayon ambapo walionekana kuelemewa kwa kiasi kikubwa katika mechi hiyo.

Hata hivyo katika kipindi cha pili wekundu wa Msimbazi waliweza kumiliki mpira kwa kipindi kirefu huku wakirusha makombora kwa mlinda mlango wa Rayon kwa lengo la kuongeza bao jingine katika timu yao lakini mashambulio hayo hayakuweza kuleta matokeo mapya. Mpaka kipenga cha mwisho kilivyopigwa uwanjani timu ya Rayon FC ilishindwa kujitutumua kurudisha bao moja walilopachikwa na wapinzani na kupelekea Wekundu wa Msimbazi kuwa washindi wa mechi hiyo.

Weka maoni