Sinahemuka – Western Boys & Mr HU

431

Lengo letu ni kukuletea nyimbo kali. Huu hapa unaitwa Sinahemuka (Siwezi kukuzingua/kukuumiza), ni wimbo wa mapenzi wa kundi la muziki la Westen Boyz la vijana watatu kutoka Mkoa wa Magharibi nchini Rwanda ambao ni pamoja na Twambazimana Aimable aka Bob, Ukwizagira David aka Stone David na Rugiramigabo Eric aka Ricky Bre wakishirikiana na Mr HU.

“Kundi letu lipo kuanzia mwaka 2014 tulipokutana shule moja ya sekondari huko wilayani Karongi tukatambua sote watatu tuna vipaji na kuamua kuunda kundi la muziki. Tulipoanza muziki tukatafakari kuhusu jina la kundi letu tukaamua kujiita Western Boyz kwani Karongi ipo Mkoa wa Magharibi. Siyo kwamba sisi ni raia wa Mkoa wa Magharibi tumejiita hivyo tu kwa kuwa tulikuwa mkoani humo, mimi nyumbani ni hapa Remera (Mjini Kigali),” amesema Bob katika mahojiano na Habari Pevu.

Ameongeza, “Kufikia leo tuna nyimbo sita ukijumlisha nyimbo zetu kama sisi na nyimbo za kushirikiana na wasanii wengine. Tunasikia watu wanatufananisha na Urban Boys eti tumefanana kiuimbaji ila hatujawaiga, wakisikiliza vizuri watagundua utofauti ila hata hivyo hiyo ya kufanana kisauti haitakiwi ilete mgongano kwani hata Harmonize si inasemekana anamuiga Diamond? Mbona hawajafarakana? Hata ikitokea umuige mtu ina maana unamkubali na kukubalika siyo jambo la baya la kuzua zogo, inaonesha unafanya kazi vizuri na watu wanapenda.”

Weka maoni