Singida United imesajili mchezaji kutoka Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini

128
Matajiri wa soka la bongo kwa sasa,Singida United wamefunga usajili kwa staili ya aina yake baada ya jana usiku kumsajili straika wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Mzimbabwe Michelle Katsavairo.
Katsavairo mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Singida United kwa mkopo wa msimu mmoja hii ni baada ya kushindwa kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Kaizer Chiefs.
Kabla ya kutua Kaizer Chiefs,Katsavairo aliwahi kutamba na vilabu vya nyumbani kwao Zimbabwe vya Platinum FC pamoja na Chicken Inn F.C.
Mbali ya Katsavairo mwingine aliyenaswa na Singida United jana ni mlinda mlango Peter Manyika Jr aliyekuwa akiichezea Simba.
Manyika amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba wake na Simba kuisha.
Wakati huohuo Singida United imemtoa kwa mkopo wa msimu mmoja kwenda Stand United nyota wake Mzimbabwe,Wisdom Mutasa.

Weka maoni