Sitegemei ulinzi wa polisi nina ulinzi wangu binafsi – Floyd Mayweather Sr

132

Baba mzazi wa Mwanamasumbwi maarufu duniani, Floyd Mayweather Jr ameshindwa kuzuia hisia zake kwenye ishu ya ubaguzi  wa rangi na kudai endapo atabaguliwa au kufanyiwa vitendo viavyoshabihiana na hivyo, kutoka kwa mtu mweupe basi atamalizana nae kwa kumtwanga makonde.

Floyd Mayweather Sr ambaye nae alitamba kwenye mchezo wa ndondi miaka ya 1970’s-1980’s, ametoa kauli hiyo kufuatia matukio mbalimbali ya ubaguzi wa rangi yanayoendelea nchini Marekani.

“Niwambie tu kuwa sitegei ulinzi wa polisi nina ulinzi wangu binafsi, hivyo kama itafikia mahala mtu mweupe ananiletea ubaguzi au vitu vinavyoshabihiana na ushenzi huo, niamini mimi nitajilinda kwa kumtwanga, sitakubali kuumizwa”,amesema Mzee Mayweather Sr kwenye mahojiano yake na mtandao wa TMZ.

Wiki iliyopita  nchini marekani mwanaume mmoja mweupe huko mjini charlottesville nchini Marekani aliendesha gari kwa kasi kwenye umati wa watu weusi waliokuwa wakiandamana na kuua mtu mmoja huku wengine 11 wakiachwa majeruhi.

Tukio hilo limelitafsiriwa kama la ubaguzi wa rangi huku watu weupe na Rais wa Marekani, Donald Trump  akidai limetekelezwa na waislamu wenye itikadi kali.

Weka maoni