Staa wa Hollywood Harrison Ford aelezwa kuhusu mauaji ya kimbari Rwanda

176
LA Premiere of 42 Arrivals

Muigizaji hodari wa filamu za Hollwood Harrison Ford amelitembelea eneo la makumbusho ya mauaji ya kimbari yaliyofanya dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994.

Alipofika makumbushoni tarafani Gisozi wilayani Gasabo, mjini Kigali, muigizaji huyo alielezewa jinsi watu zaidi ya miliyoni moja walivyouawa kinyama katika kipindi cha miezi mitatu tu.

Baada ya kuweka shada la maua makaburini, staa huyo alidai kusikitishwa na yaliyowasibu wanyarwanda, na kuwapongeza kwa jitihada zao kutunza ushahidi wa historia hiyo.

Ameongeza, “Kazi mnayoifanya itaijenga dunia. Tunajiunga nanyi katika maombolezo na tunathamini sana juhuzi zenu katika kujenga umoja.”

Harrison Ford, 74, alijiulikana kupitia filamu lukuki alizoigiza mathalani ’Blade Runner’ (mwaka 1982), ’The Fugitive’ (1993); ’Air Force One’ (1997); ’Raiders of the Lost Ark’ (1981) na nyinginezo nyingi.

Weka maoni