Tanzania yajipanga kwenye maingilio ya watu

93

Serikali imesema njia za maingilio yote rasmi hapa nchini yaani angani, majini na nchi kavu yapo salama na itaendelea kuhakikisha yanakua katika hali hiyo hiyo huku ikiwahakikishia wageni mazingira bora ya kufanya shughuli zao hapa nchini.

Manaibu mawaziri watatu akiwemo wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Hamad Yusufu Masauni ,wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Edwine Ngonyani na wa Maliasili na Utalii Mh. Ramo Makani wameyasema hayo katika ziara yao ya pamoja ya kukagua maingilio rasmi ya watu nchini.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Hamad Yusufu Masauni amesema wizara yake imekua ikifanya kazi zake kikamilifu katika kuwafanya wageni wanaoingia hapa nchini ni wema na wanafuata taratibu za nchi kwa kipindi chote cha uwepo wao nchini.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Edwine Ngonyani amesema wizara hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali walioko chini yake katika kuifanya miundombinu ya hapa nchini inakua rafiki kwaajili ya matumizi kwa wageni hapa nchini na wenyeji.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Ramo Makani amesema wizara yake imeamua kushirikiana na wizara zingine katika kuangalia jinsi ya kuboresha sekta mbalimbali ili idadi ya watalii waingiao hapa nchini inaongezeka.

Weka maoni