Tarehe ya kurudia uchaguzi nchini Kenya yatajwa rasmi

223

Baada ya Mahakama ya juu kufuta matokeo ya uchaguzi nchini Kenya, hatimae Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini humo (IEBC), imetangaza tarehe mpya ya kurudia uchaguzi huo. uchaguzi mpya wa urais nchini humo utafanyika tarehe 17 Oktoba mwaka huu.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati amesema uchaguzi huo utarudiwa tarehe 17 Oktoba mwaka huu na utashirikisha wagombea wawili pekee wa urais, ambao ni Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga kupitia tiketi ya umoja wa vyama vya upinzani (NASA).

Weka maoni