The Ben na Sheebah waachia wimbo wao wa ‘Binkolela’

552

Msanii The Ben wa Rwanda na Queen Sheebah Karungi wa Uganda wameachia wimbo walioshirikiana ambao unaitwa ‘Binkolela’, ambapo umetengenezwa nchini Uganda.

Video ya wimbo huo ilifanyiwa shooting nchini Afrika Kusini mwaka jana.

Wimbo huo jana ndipo ulipandishwa mtandaoni kwenye channel ya lebo ya Press One ambayo kwa kawaida ndio inasimamia kazi za The Ben anakoishi huko Marekani.

Mtayarishaji wa muziki ambaye ni maarufu nchini Uganda aitwaye Nessim ndiye ametengeneza wimbo huo wa Binkolela.

The Ben ni Mnyarwanda ambaye anakaa Marekani tangu mwaka 2010. Alikuja nchini Rwanda mwishoni mwa mwaka jana kwa ajili ya tamasha la East African Party.

Kabla ya kurundi makwake Marekani kuna shoo aliyoshirikiana na Sheeban nchini Uganda, ambapo siku hizo ndipo hata aliposhirikishwa kwenye collabo ya ‘Kami’ ya msanii Kid Gaju.

The Ben ni miongoni mwa nguzo muhimu za muziki wa Rwanda. Anafanya muziki wa RnB na Pop.

Sheebah alijizolea umaarufu mkubwa nchini Uganda hasa kutokana na wimbo wa Farmer alioshirikishwa na Ykee Benda ambao unafanya vizuri nchini Rwanda.

Weka maoni