Tony B akanusha kusaka kiki kwa Diamond, Tijarat, Anita, Gahongayire, Doriane

270

Msanii anayechipukia nchini Rwanda Tony B amekanusha kutafuta kiki kwa watu maarufu nchini kupitia wimbo wake wa ‘Tamaa yangu’ ambapo anayataja majina ya mastaa wengi.

Katika wimbo huo amewataja kwa majina watangazaji maarufu nchini Rwanda akiwemo Tijarat Kabendera, Anto Niyongira, Anita Pendo akisema anatamani kuwa nao.

Amemtaja pia Aline Gahongayire, Miss Rwanda 2015 Kundwa Doriane, akisema hao wote anawapenda na anahisi tamaa yake itakuja kumponza kama Mungu hatamnusuru.

Akizungumza na Habari Pevu, Tony B amesema wimbo wake umejaa ubunifu, kitu ambacho wasanii wa Rwanda hawana, na kukanusha kutafuta kiki kwa mastaa.

Msikilize hapa

 

Weka maoni