Trump adaiwa kufichua siri za Marekani kuhusu ISIL kwa Urusi

212
Lavlov na Trump

Gazeti la The Washington Post linadai limezipata habari kuhusu Rais Donald Trump kufichua siri za Marekani kuhusu kundi la kigaidi la Islamic State kwa Urusi.

Donald Trump amedaiwa kumwaga siri hizo kwa Waziri wa Nchi za Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, walipokutana kwa mazungumzo May 10, 2017.

The Washington Post wamesema taarifa za ufichuaji wa siri za Marekani zimetolewa na viongozi walio katika Serikali ya Marekani wengine ambao hawamo tena.

Imeripotiwa Trump alipokutana na Lavrov na Balozi wa Urusi nchini Marekani, aliongea hadi mambo ambayo alikuwa hajapangiwa kuyazungumzia, yawezayo kuhatarisha usalama wa Marekani.

Hata hivyo, Rais wa Mamlaka kisheria anaruhusiwa kuamua nini ni siri kuu na nini ni siri za kawaida, ikiwa na maana kwamba hajavunja sheria yoyote, kwa mujibu wa The Washington Post.

Kashfa hii inaripotiwa siku chache baada ya Trump kumpiga kalamu Mkuu wa FBI James Comey, ambaye alikuwa anachunguza uhusiano wa Trump na Urusi wakati wa kampeni yake ya kusaka urais.

Ikulu ya Marekani imesema habari hii ya The Washington Post ni uongo, ikisema Trump hajaongea vitu ambavyo ni siri.

Ripoti ya Washington Post inasema waliokuwepo katika kikao hicho ambacho trump alifichua siri, walizima moto kwa kuwafahamisha maafisa wa CIA na wale wa NSA.

Weka maoni